Mambo 10 usiyoyajua
kuhusu watoto wachanga.
Makala haya yameandaliwa kutokana na mahojiano
yaliyofanyika kati ya mtaalam wa afya ya watoto kutoka katika Chuo Kikuu cha
Tiba cha Malawi – Blantyre (Malawi University College of Medicine).
1. Choo chao cha
kwanza huwa hakinuki.
Choo chao cha kwanza chenye muonekano wa kama lami, kina ute na
majimai kutoka tumboni pamoja na chochote kile wanachokuwa wamekula wawapo
tumboni mwa mama zao na mara nyingi choo hiki huwa hakinuki. Huwa bado
hakijapata bakteria wa tumboni ambao hufanya choo kinuke. Lakini kitaanza
kunuka punde baada ya bakeria kuenea tumboni. Baada ya siku moja au mbili choo
chake kinakuwa cha kijani kisha cha njano na baadae rangi ya hudhurungi ambayo
ni rangi yake asili.
2. Huwa wanalia
bila machozi, kwa mara ya kwanza.
Watoto wachanga wana anza kulia kuanzia wiki ya 2-3 lakini
machozi yana anza kutoka baada ya kuwa wamefikisha mwezi mmoja. Wakati wa
alasiri na jioni ndio wakati wanaopenda kuwa wasumbufu, bila sababu ya msingi
na hakuna utakachoweza kufanya kuwatuliza.
"Kipindi cha watoto kulialia zaidi" ni katika wiki ya
46 hivi baada ya kujifungua au mtoto akiwa na wiki 6 mpaka 8 kwa watoto
waliozaliwa wakiwa wametimiza umri wa kuzaliwa. Baada ya miezi 3, tufani huwa
imepita.
3. Wakati
mwingine watoto wachanga wanaweza kuacha kupumua kwa muda.
Watoto wachanga wanaweza kuacha au kukoma kupumua kwa sekunde 5
mpaka 10 hususani wanapokuwa wamelala kitendo ambacho hutosha kumfanya mzazi
yeyote yule kuchanganyikwa. Ila huna sababu ya kutahayari, lakini kama mwanao
atakoma kwa muda mrefu zaidi au kama atabadilika na kuwa wa bluu. Hiyo ni
dalili ya hatari, tafuta msaada wa kitabibu haraka iwezekanavyo.
Lakini kama hali hii pia inaweza kujitokeza baada ya motto kushtushwa
au baada ya kulia.
4. Watoto wa
kiume huwa wanasimamisha uume wao.
Kitendo ambacho mara nyingi huwa kinatokea pale anapokuwa anataka kukojoa. (Hii inaweza
kuwa ni dalili nzuri ya kuangalia kama mtoto ni mzima).
Unaweza kuona wakati unapokuwa
ukimbadilisha mwanao daipa, nepi ama kumpeleka kujisaidia. Sababu hasa ya
kusimamisha uume wakati wa kukojoa haijulikani, hata hivyo siyo jambo la
kutahayari au kuonea haya. Unaweza kuona hili kupitia kipimo cha ultrasound kabla mwanao hajazaliwa.
Uume wake unaweza kuonekana mkubwa wakati wa kuzaliwa, hata hiyo
pia ni jambo la kawaida.
5. Watoto
wachanga huwa matiti makubwa.
Wanapozaliwa kwa mara ya kwanza wote watoto wa kiume na kike
huwa wanaonekana kama wana matiti makubwa kuliko inavyotarajiwa.
Na wakati mwingine matiti haya huwa
yanatoa maziwa.
Kwenye chuchu zao kumefanyika vibonge,
kwa sababu ni vichocheo vya estrogeni kutoka kwa mama na vitapotea vyenyewe
baada ya wiki chache.
Pia kwa Watoto wa kike wanaweza kuwa wanatokwa na hedhi
ndogo au maji maji kutoka ukeni nayo hayo yatapotea baada ya siku chache.
6. Mafindofindo (tonsils) yao
yanakuwa yana tezi kwa ajili ya kutambua ladha ya chakula.
Mtoto mchanga anakuwa na tezi za kutambua ladha ya chakula, ambazo
huwa na ukubwa sawa na zile walizonazo vijana wadogo.
Tofauti kubwa ni kuwa tezi za vichanga
zimechukua eneo kuwa zaidi hadi kufika kwenye mafindofindo hadi nyuma ya koo.
Mtoto mchanga anaweza kuonja vitu vitamu, vichungu, vichachu ila bado hawezi
kuitambua ladha ya chumvi kwani ladha hii ni mpaka miezi mitano.
7. Hupenda kulala
kuelekea upande wa kulia.
Ni asilimia 15 ya watoto wachanga wanaopenda kuelekeza uso wao
upande wa kushoto wanapaolalia mgongo. Inaoenekana ina uhusiano na jeni (gene)
kama ilivyo kwa kitobwe(dimples). Tabia hii ya kupenda kulala kuelekea upande
wa kulia inachukua miezi kadhaa kabla ya kupotea, na hata hivyo inaweza pia
kusaidia kuelezea kwa nini watu wengine ni mashoto au wengine hutumia mkono wa
kulia.
8. Wana kiwango
kikubwa cha baadhi ya seli za ubongo.
Ubongo wa mtoto mchanga utakuwa mara mbili zaidi katika mwaka wa
kwanza. Ubongo huu unakuwa tayari una seli za neva nyingi zaidi ya zile za mtu
mzima ambazo zina uwezo wa kubeba taarifa za fahamu. Seli nyingi huwa zinakufa
na seli chache zinazalishwa.Na baada ya kuwa mtu mzima unajikuta una seli chache
za neva kuliko ulivyokuwa mtoto. Na muunganiko kati ya seli moja na nyingine
huwa unapunguzwa kitu ambacho husaidia kuongeza umakini lakini hunapunguza
ubunifu.
Watoto ni wabunifu kuliko watu wazima.
Hili
Halipingiki.
9. Wanaweza
kujishitua wenyewe.
Siyo jambo gumu kushituka kwa mtoto mchanga: - sauti kubwa,
harufu kali, mwanga mkali, mtikisiko wa ghafla na hata kulia kwao wenyewe
kunaweza kuwashitua. Utajua hivyo vyote pale atakapokuwa akitupa mikono yake
pembeni huku akiwa amekunjua viganja vyake kisha kwa haraka akikunja vinganja
vyake na kuipeleka nyuma ya mwili wake.
10.
Baadhi ya alama za kuzaliwa zitapotea.
Alama ya kung'atwa na korongo (Stork bites) au "busu la
malaika" la rangi nyekundu au pinki mara nyingi kwenye paji la uso, kwenye
kope za macho au kwenye sehemu ya nyuma ya shingo ikiwa ni pamoja na doa la
kimongolia - doa la bluu ambalo huonekana kama wino uliovia mgongoni au kwenye
matako. Hili hupotea ndani ya miaka michache. Chanzo chake hakijulikani.
Alama ya rangi nyekundu iliyokolea kama ya stroberi hutokana na
mishipa ya damu inayokua kwa kasi. Hizi alama hutokea baada ya wiki nyingi na
huchukua miaka kadhaa kupotea.
Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116 ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa