MwanaspotiJul 29, 2021
Nafasi ya Manara imezibwa na mwanahabari Ezekiel Kamwaga ambaye atakaimu kwa miezi miwili.
Kupitia mtandao wa Instagram, Manara ameweka picha akiwa ameshika begi akitembea na kuandika neno kubwa kwake ni Alhamdulillah akimaanisha anamshukuru Mungu.
Ameandika; "Kila tunapomaliza Mechi yoyote ile ya Simba, neno langu la kwanza baada ya matokeo yoyote yale ni Alhamdulillah.
Kwa wanaofuatilia page hii wanatambua hilo. Kwangu neno hili ndio Msamiati nnauotumia mara nyingi zaidi na hufanya hv kwa kila jambo ,liwe jema au baya. Yes neno langu ni moja tu
AL-HAMDULILLAH"