Breaking News

 KUTOKA GAZETI LA NIPASHE MWANGA WA JAMII

Wanawake jamii wafugaji watakiwa kuvunja ukimya

WANAWAKE wa jamii za kifugaji katika Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha, wameshauriwa kuvunja ukimya na kufichua vitendo vya ukatili wa kijinsia kama vipigo, ndoa za utotoni, ulawiti na ubakaji ili serikali ichukue hatua ya kuwafikisha wahusika mahakamani.


Wanawake jamii wafugaji watakiwa kuvunja ukimya

WANAWAKE wa jamii za kifugaji katika Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha, wameshauriwa kuvunja ukimya na kufichua vitendo vya ukatili wa kijinsia kama vipigo, ndoa za utotoni, ulawiti na ubakaji ili serikali ichukue hatua ya kuwafikisha wahusika mahakamani.

Pia, wameshauriwa kukataa utamaduni wa kumaliza kesi hizo kienyeji hasa kimila, badala yake watafute haki yao kwa kuripoti kwanza matukio hayo polisi ili yafikishwe mahakamani.

Ushauri huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Shirika la Emimutie Women Organization, Rose Njilo, wakati akizungumza na wadau wa masuala ya ukatili wa kijinsia wilayani humo.

Alisema shirika hilo, limeamua kuvalia njuga suala la ukatili wa kijinsia hususani masuala ya ukeketaji na ndoa za utotoni unatokomezwa.

“Emimutie, tumeamua kuvalia njuga suala la ukatili wa kijinsia na tunataka kuhakikisha watoto wanasoma na kupata haki zao za msingi hususani katika jamii ya kifugaji tunapambana kuhakikisha masuala ya ukatili yanatokomezwa,” alisema Njilo.

Kabla ya kikao hicho, shirika hilo liligawa taulo za kike kwa watoto zaidi ya 300 wa shule mbalimbali za wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Raymond Mangwala, aliwataka wakazi wa wilaya hiyo kufahamu kuwa wale wote watakao kaidi kupeleka watoto wao shule wajiandae kukumbana na mkono wa sheria.

“Elimu bure bado ukatae kumpeleka mtoto shule? Utaeleza kwanini umekatili agizo la serikali lakini pia nitoe rai kwa vijana wanaobaka watoto wa shule katika wilaya yangu sitafumbia macho miaka 30 itawahusu jela bila kupepesa macho,” alisema Mangwala.

Aidha, aliwataka wananchi hao kuheshimu haki za wanawake pamoja na watoto wa kike ili kuleta usawa wa kijinsia katika jamii hiyo.

Mmoja wa wakazi wa wilaya hiyo, Mariana Jacob, alisema wasichana hasa wa jamii ya kifugaji, wanalipiwa mahari wakiwa bado wadogo na hivi sasa wanalazimishwa kuolewa wakiwa bado hawajamaliza masomo.

Alisema kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa kutaleta manufaa mengi ikiwamo upatikanaji wa huduma za kijamii, kwamba waondoe fikra potofu kwamba kuhesabiwa kunaleta uchuro.

Alisema ofisi yake imeshapokea barua ya maelekezo kutoa mkoani kuhusu uhamasishaji wa zoezi hilo.

Bulembo alisema kuwa maandalizi ya zoezi hilo yataanza kufanyika Julai, mwakani, huku akitoa maagizo kwa madiwani hao kwenda katika kata zao kuwahamasisha wananchi.

Alisema kuwa diwani ndiye mwenyekiti wa shughuli hiyo kwa upande wa kata, katika kijiji kiongozi ni mwenyekiti wa kijiji.

Alisema katika ngazi ya kitongoji kiongozi wake ni mwenyekiti wa kitongoji, katika ngazi ya wilaya kiongozi ni mkuu wa wilaya na katika ngazi ya mkoa mkuu wa mkoa ndiye kiongozi wa shughuli hiyo.

Bulembo alisema kuwa kuanzia ngazi ya kitongoji, kijiji, kata, tarafa mpaka wilaya wote wanajukumu la kuhakikisha wanahamasisha wananchi kushiriki katika zoezi la sensa.

Aidha, aliwakumbusha wananchi wa Muheza kuendelea kuchukuwa tahadhari ya ugonjwa hatari wa corona kunawa mikopo kwa maji na sabuni, kutumia vitakasa mikono, kuvaa barakoa na kuepuka


Shirika la Ndege Ufaransa kuuimarisha utalii Zanzibar

SHIRIKA la Ndege la Ufaransa limeanza safari zake za kupeleka abiria Zanzibar, ndege yake ikiwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ikiwa na abiria 175 juzi.

Mapokezi ya ndege hiyo aina ya Boeing 787-9 yalifanyika chini ya mapokezi ya mawaziri watano wa Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili kwa ndege hiyo kiwanjani hapo, Waziri Mbarawa alisema shirika hilo miaka ya nyuma lilikuwa linafanya safari zake Zanzibar lakini likasitisha na kwa sasa historia mpya imeandikwa na hivyo kuonyesha kuwa wadau wa maendeleo wana imani Serikali ya Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema serikali zote mbili zitaendelea kujipanga kuhakikisha zinawekeza katika miundombinu mizuri na ya kisasa ili kuyafanya mashirika ya ndege mengi kufika Tanzania ikiwamo Zanzibar.

Alisema ujio wa ndege hiyo ni fursa kubwa, hivyo kuwataka wale wote watakaopata fursa ya kuhudumia shirika hilo na mashirika mengine, kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa ili watalii wengi kufika na kuchangia uchumi wa nchi.

Waziri wa Biashara za Nje na Uchumi wa Ufaransa, Franck Reister, alisema usalama wa abiria ni jambo muhimu kuhakikisha kwa muda wote wanapokuwa nchini wanakuwa salama huku wakifanya shughuli zao kwa utulivu.

Alisema Zanzibar inayo nafasi kubwa ya kupiga hatua katika maendeleo ya sekta ya utalii kutokana na kuwa na vivutio mbalimbali vinavyotoa nafasi kwa wageni hao kuja mara kwa mara nchini.

"Shirika la Ndege la Ufaransa limerudisha tena huduma za usafiri kwa abiria katika kisiwa cha Zanzibar baada ya kuridhishwa na mazingira ya utulivu na usalama wa wageni wake," alisema.

Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar, Omar Siad Shabani, alisema ujio wa ndege hiyo utaleta wageni kwa ajili ya utalii, uwekezaji na biashara huku akilipongeza shirika hilo kwa kuamua kurejesha safari zake Zanzibar.

Alisema serikali itawahakikishia kila aina ya msaada wanaohitaji katika kuhakikisha uwapo wao unakuwa mzuri na wa kibiashara kwa pande zote mbili.

“Matumaini yangu kwamba siku zijazo kampuni hizi pia zitafikiria kuanza kuleta ndege za mizigo ili kuifufua Zanzibar kibiashara hasa ikizingatiwa kuwa wafanyabiashara wengi wanalalamika upatikanaji wa safari za ndege, hivyo ujio wa ndege hizo itaifungua Zanzibar kibiashara," alisema.

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Lela Muhamed Mussa, alisema ndege hiyo itafanya safari zake Zanzibar siku mbili kwa wiki ambapo kwa safari moja itakua na abiria 175, akiitaja ni hatua kubwa kwa Zanzibar.

Alisema uwapo wa ndege hiyo itakuwa ni fursa kubwa sana Zanzibar kurudi katika soko la utalii ambalo ni sekta mama inayochangia pato la taifa.

Alisema Serikali ya Zanzibar itaendelea kuchukua tahadhari ya corona ili kuwaweka salama wageni wote wanaofika nchini na kuchukua hatua za kiusalama.



Wazazi wanaoficha watoto kuanza shule kufikishwa kortini

MKUU wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha, Nurudin Babu, amesema hatosita kuwaburuza kortini, wazazi na walezi wanaotoka jamii za kifugaji ambao watakaidi amri halali ya kuwaandikisha shule watoto wenye umri wa kuanza darasa la kwanza mwaka ujao.


Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo, waliojitokeza katika mahafali ya saba ya Shule ya Sekondari ya Tingatinga iliyopo Tarafa ya Enduimet.

Alisema imebainika kuwa watoto wengi wanaoanza shule hiyo malengo yao hayatimii kutokana na utoro na wengine kuozwa katika umri mdogo.

“Utoro huu unatokana na watoto kuacha masomo na kukimbilia nchi jirani ya Kenya, kwa ajili ya kufanya kazi. Mtoto yeyote mwenye umri chini ya miaka 18 anayesoma ni marufuku kuacha masomo, ila ambaye hayupo kwenye umri wa masomo, akitaka kwenda popote aende,” alisema Babu.

Kuhusu matatizo yanayoikabili shule hiyo ikiwamo ukosefu wa uzio, Babu alisema atafanya mazungmzo na menejimenti ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, kuwaomba fedha za ujirani mwema zisaidie ujenzi wa shule hiyo iliyopo kwenye hifadhi na mapito ya wanyamapori.

Awali, Mkuu wa Shule hiyo, Pantaleo Paresso, alisema wahitimu hao walianza masomo wakiwa 297, lakini wanaohitimu 271, huku sababu kubwa ikiwa ni utoro na wengine kuhama.

"Hali ya ufaulu kwa miaka miwili ya nyuma ilikuwa nzuri. Mwaka 2019 tulifaulisha kwa asilimia 87, 2020 sawa na asilimia 94, na tunatarajia mwaka huu kufaulisha kwa asilimia 100,"alisema Paresso.

Alisema shule hiyo inatarajia kutoa mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), baada ya jengo na vifaa kukamilika kwa gharama ya Sh. milioni 103, lakini tatizo lililopo hakuna mwalimu wa TEHAMA.

Asilimia 100 ya Shule za sekondari za wilayani hiyo ni za bweni, lakini hazina uzio na mazingira ya shule hizo ni magumu.

Mbunge wa Longido, Dk. Steven Kiruswa, aliwahi kusema katika jitihada za kuhakikisha uzio unapatikana kwa shule hizo, amepata mbegu ya mchongoma ya muda mfupi itakayoweza kuoteshwa kuzunguka mipaka ya shule ili kuwa na uzio wakati serikali ikijipanga kujenga uzio imara.


 KUTOKA GAZETI LA MWANANCHI

Kimeta yadaiwa kuua wawili, 30 walazwa Kilimanjaro


kimetapicMkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai

Watu wawili wakazi wa wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro wamefariki dunia baada ya kula nyama ya ng'ombe anayesadikiwa kuwa na ugonjwa wa kimeta huku wengine zaidi ya watu 30, wakilazwa hospitalini.

Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mtu mmoja anayedaiwa kujifanya mtaalamu wa mifugo na kuthibitisha nyama hiyo ni salama, mtu huyo yupo mahututi katika Hospitali ya Ngoyoni Rombo.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Oktoba 21, 2021 na Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai, amesema watu hao walikula nyama hiyo Oktoba 6, 2021 baada ya mtu aliyejifanya mtaalamu wa mifugo kuthibitisha nyama hiyo ni salama na kuipiga mihuri feki.

Kagaigai amesema zaidi ya watu 30 waliokula nyama hiyo waliathirika ambapo wawili wamefariki dunia, huku wengine wakiendelea na matibabu katika Hospitali ya Ngoyoni iliyopo Wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.

"Oktoba 6, 2021, eneo la Mamsera, nyumbani kwa mwananchi mmoja, kulikuwa na Ng'ombe watatu na mmoja alikufa, mtu moja alijitokeza kuwa ni mtaalamu wa mifugo akathibitisha ng'ombe yule alikuwa mzima hana matatizo akagonga na mihuri ambayo nafikiri ilikuwa feki,"amesema RC Kagaigai.

"Baada ya kuchinja, mtu yule alianza kuugua, na waliokula nyama ile wote wakaanza kuugua, ikawekwa mashaka na walipofuatilia ikaonekana kuna dalili za kimeta,"amesema na kuongeza kuwa tayari Serikali imechukua hatua mbalimbali.

Miongoni mwa hatua hizo ni kuiweka karantini mifugo yote iliyopo kwenye familia hiyo na akaongeza kusema kuwa kuna uwezekano wa kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa Kimeta, na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari ikiwemo kuepuka kula nyama za mizoga kutokana na hofu ya ugonjwa huo.

"Nitoe tahadhari kwa wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro hususani Wilaya ya Rombo, kujiepusha kula nyama ya mizoga, kutokana na tukio hili, lakini Serikali bado tunaendelea na uchunguzi, ili kujua kama ni Kimeta au vinginevyo,"amesema.

Mkuu huyo wa Mkoa, alitumia pia nafasi hiyo, kuwataka wananchi na wale wote wenye mabucha ya nyama mkoani humo, kuhakikisha nyama hizo zimepimwa na mtaalamu wa mifugo aliyethibitishwa.


Sabaya, wenzake wawasilisha kusudio la kukata rufaa

THURSDAY OCTOBER 21 2021

sabayapic

  

Arusha.

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wamewasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo Alhamisi Oktoba 21, 2021 ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha Oktoba 15.

Katika kesi hiyo Sabaya na wenzake watatu wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Post a Comment

أحدث أقدم
Contact ME
close