Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 02.10.2021: Sterling, Vlahovic, Haaland, Werner, Ndombele, Torres, Tuanzebe
Mshambuliaji wa Fiorentina na Serbia Dusan Vlahovic, mwenye umri wa miaka 21, ana ndoto za za kuhamia katiika Manchester City. Klabu hiyo ya Championi ya Primia Ligi ilihusishwa na uhamisho wa mchezaji huyo katika kipindi cha msimu uliopita (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Meneja wa Manchester Ole Gunnar Solskjaer amemwambia winga wa England mwenye umri wa miaka 21 Jadon Sanch kuwa mkweli, wakati akisubiri bao lake la kwanza katika klabu hiyo. (Mirror)
Mshambuliaji wa Chelsea na Ujerumani Timo Werner, mwenye umri wa miaka 25, anakabiliana nakupambania hali yake ya baadaye katika klabu hiyo baada ya kuhangaika kuimarika katika klabu hiyo tangu kuwasili kwa Romelu Lukaku. (London Evening Standard)
Manchester City wanaangalia kuwezekano wa kufanya dau na mlinzi wa Villarreal na Uhispania Pau Torres, mwenye umri wa miaka 24. (Marca - in Spanish)
Jose Mourinho anapanga mpango wa kushitukiza wa kukutana tena na shambuliaji wa Tottenham Mfaransa Tanguy Ndombele, 24, katika Roma. (Calciomercarto via Express)
Huenda Everton wakamnunua kiungi wa kati wa Newcastle Muingereza Sean Longstaff, mwenye umri wa miaka 23. (Independent)
Real Madrid watakuwa na pesa za kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Erling Haaland, mwenhye umri wa maika 21, msimu ujao, huku wakiendelea kuwa na nia ya kumnunu nyota wa Paris St-Germain na Ufaransa France star Kylian Mbappe, mwenye umri wa miaka 22. (AS - in Spanish)
Mlindi wa Uingereza Axel Tuanzebe, mwenye umri wa miaka 23, yuko wazi kuufanya mkataba wake wa mkopo katika Aston Villa kutoka Manchester United kuwa wa kudumu. (Birmingham Mail)