Breaking News

 

WAKATI joto la pambano la watani wa jadi Simba na Yanga likianza kupanda wenyeji wa mchezo huo Simba imetoa kauli nzito ikisema hawako tayari kuwaona wapinzani wao wanatangaza ubingwa mbele yao.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja mawasiliano wa Simba Ahmed Ally akisema kuelekea mchezo wa Aprili 16  klabu yao haitakuwa tayari kugeuzwa ngazi ya Yanga kuufuata ubingwa.

Ahmed amesema hata kama Simba itakosa ubingwa lakini wamewaambia wachezaji wao kuwa jambo la Yanga kushinda mbele yao wakati wakielekea kuchukua ubingwa halikubaliki.



"Hii historia mbaya tukiiruhusu itaishi vizazi na vizazi,Simba haiwezi kukubali hili litokee, tutakuwa na dakika tisini za kwenda kulinda heshima ya Simba mbele ya watani wetu,"amesema Ahmeid ambaye klabu yao ipo nafasi ya pili kwenye msimamo.

"Tumewaambia wachezaji wetu kwamba huu ni mchezo mkubwa kuliko yote na matokeo yake yatatupa heshima au kutubomoa lakini kubwa hatutakubali kugeuzwa ngazi ya ubingwa na Yanga.

Yanga ambao ndio vinara wa msimamo wa ligi wanakutana na Simba huku mabingwa hao watetezi wa ligi endapo watashinda mchezo huo wa Jumapili itahitaji ushindi wa mchezo mmoja pekee kuwa mabingwa.

Post a Comment

أحدث أقدم
Contact ME
close