Breaking News


 

Ukweli ni kwamba,upungufu ama kupungukiwa Nguvu za kiume siyo ugonjwa,kama wengi tunavyo dhani,ila ni dalili tu,ambapo mwili hukujulisha kuwa wewe ni mgonjwa.

Hii ni taarifa kuwa mwili wako una dosari au kuna udhaifu wa kiutendaji ndani ya mwili wako,

Kuna sababu takribani 200 zinazompeleke mwanaume kuwa na upungufu wa nguvu za kiume.

Unaweza kujiuliza kwa nini kuwe na sababu nyingi kiasi iko?

Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Ni Nini?

Nguvu za kiume ni nomino ya kiujumla yenye vipengele vingi vyenye mwambato wa maneno ikiwemo ni;

-Pamoja na hamu ya mapenzi

-Kusimama kwa uume barabara

-Kuchelewa kufika kileleni kiasi cha kufurahia tendo la ndoa

-Uwezo wa kurudia tendo la ndoa

-Pumzi,wepesi na uchangamfu wa mwili katika kutenda tendo la lenyewe.

Ni Viungo Gani Mahususi Hususani Kuajili Ya Nguvu Za Kiume?

Nguvu za kiume ni jambo pana sana linalo husisha viungo na vitu vingi ndani ya mwili.

Kuna zaidi ya viungo na vitu 50 ndani ya mwili wa mwanaume vinavyohusika na nguvu za kiume ambapo viungo hivi pia hufanya kazi zingine za mwili.

Baadhi ya viungo hivyo ni ubongo, moyo, mishipa ya neva,mishipa ya ateri zote,mirija iliyo ndani ya uume iitwayo corpora cavernosa.

Viungo vingine ni neva maalumu za parasympathetic,tezidume (prostate gland), ini, figo, homoni ya testestorone, kemikali za acetylcholine, serotonin, na dopamine, uti wa mgongo, eneo la chini ya mgongo (kiuno), eneo la nyonga.

Viungo vingine ni misuli maalumu iitwayo pelvic floor, tezi pituitari (pituitary gland), utando maalumu wa uumeni uitwao tunica albuginea, misuli iitwayo pubococ ygeus [PC muscles],kemikali ya nitric oxide, kemikali ya prolactin kn.

Nini Maana Ya Upungufu Wa Nguvu Za kiume?

Unapo pungukiwa(Upungufu),wa nguvu za kiume ina maana ndani ya mwili wako kuna baadhi ya vitu,hususani nilivyovitaja hapo juu havifanyi kazi vizuri ipaswavyo,yawezekana ni figo ndilo halifanyi kazi vizuri,au ini, au tezi dume, au neva ya parasympathetic, au moyo una tatizo au mishipa ya ateri, au misuli ya pelvic au homoni fulani iko juu sana au iko chini sana (hormonal imbalance), orodha ni ndefu sana sana.

Kitendo cha baadhi ya viungo hivyo kutofanya kazi vizuri basi hapo ndipo neno Upungufu wa Nguvu za kiume hutokea.

Upungufu huo unaweza kuwa ni:

1. Kukosa hamu ya mapenzi

2. Uume kusimama kwa uregevu

3. Kuwahi kufika kileleni

4. Kuchelewa sana kufika kileleni (au kushindwa kufika kileleni kabisaa)

5. Kushindwa kurudia tendo la ndoa

6. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo

7. Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji

8. Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu.

Kwa faida yako wewe msomaji, ili uelewe vizuri zaidi labda niseme kwamba, nguvu za kiume ni kiwanda,na ni zaidi ya kiwanda.

Ndani ya kiwanda kuna umeme, maji, madawa, watu (wafanyakazi wa kila taaluma na fani), mashine, mitambo n.k.

Mfano ikatokea kukawepo na ukosefu wa kitu kimojawapo,mathalani umeme, au wafanyakazi wakagoma, au kukakosekana madawa muhimu au maji na kadha wa kadha, basi bidhaa inayotarajiwa kupatikana sokoni, kwa hakika haitapatikana.

Vivyo hivyo nguvu za kiume, mathalani, ikitokea tezi dume kutofanya kazi vyema, basi hapo mwanaume hatoona nguvu za kiume, zitapungua au zitaisha kabisa!

Kwa hiyo upungufu wa nguvu za kiume ni upungufu au kasoro za kiutendaji wa viungo ndani ya mwili wa mwanaume.

Mwanaume yoyote anapaswa kutambua jambo hili.

Tujiulize Nini Kinachopelekea Viungo Hivyo Vishindwe Kufanya Kazi Vizuri?

Kuna maradhi kadhaa,vyakula tunavyokula, tabia na mtindo wa maisha vinavyoweza kupelekea viungo hivyo kutofanya kazi vizuri.

Baaadhi ya maradhi hayo na tabia hizo ni;

-Kujichua/punyeto (masturbation)

-Kisukari

-Presha ya kupanda

-Presha ya kushuka

-Uvutaji wa sigara

-Unywaji wa pombe

-Madawa ya kuleva

-Kufanya kazi kupita kiwango na kukosa muda wa kupumuzika

-Matatizo ya kukosa usingizi na kuchelewa kulala usiku.

Sababu Zingine Za Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Ni;

Kutokunywa maji ya kutosha, tatizo la kutopata choo hasa pale unapotumia nguvu nyingi kusukuma choo.

Kutofanya mazoezi,ukosefu wa kumbukumbu,uzito mkubwa/unene mkubwa,kitambi,kuvimba kwa tezidume (Benign Prostate Hyperplasia).

Sababu zingine ni saratani ya tezi dume (Prostate cancer), matibabu ya mionzi ya tezidume na upasuaji,ugonjwa unaoathiri vitendo na shughuli za mwili kama vile mwondoko na balansi (multiple sclerosis), ugonjwa ambao hudhuru mawasiliano ya ubongo na miondoko ikiwa ni pamoja na kutembea, kuongea na kuandika (parkinson’s disease), vyakula vya mafuta, vyakula vilivyowekewa homoni bandia za kike n.k.

Sababu zingine ni maumivu ya mgongo/kiuno; baadhi ya madawa ya kemikali (madawa ya hospitali); kiharusi (stroke); upungufu katika utendaji wa kazi za gonadi (hypogonadism); uzalishaji mwingi wa homoni ya thyroid.

Sababu zingine ni kutozalishwa kwa homoni ya thyroid ya kutosha; ugonjwa unaoathiri uzalishaji wa homoni ya cortisol (cushing’s syndrome); ugonjwa wa kupinda uume (peyronie’s disease); kukakamaa kwa mishipa ya damu (atherosclerosis); orodha ni ndefu sana, ni zaidi ya 200.

Hivyo mwanaume anapopungua nguvu za kiume, ina maana kuna ugonjwa ndani ya mwili wake, au unaweza kuwa huo ugonjwa umeshadhihirika (umeshatokeza) kwa nje, au huo uko ndani ya mwili unamla na kummaliza kimyakimya kama yalivyo baadhi ya magonjwa ambapo baadaye hulipuka.

Hii ndiyo maana kitaalamu tunasema kupungua nguvu za kiume siyo ugonjwa ni dalili ya ugonjwa.

Unapo pungukiwa nguvu za kiume hiyo ni ISHARA YA TAHADHARI kwamba ndani ya mwili wako kuna kitu hakifanyi kazi kwa Ufasaha.

Unashauriwa kuchukua TAHADHARI kabla makubwa hayajakufika.

SASA HAPA WANAUME WENGI TUNAPOTOKA...!!

Wanaume wengi wanapo pungukiwa nguvu za kiume hukimbilia kutafuta dawa za kuongeza nguvu za kiume, na siyo kutibu.

Hili ni KOSA TENA,KUBWA sana!

Ni kosa kubwa kukurupuka kubugia dawa za nguvu za kiume bila kujua chanzo cha tatizo na bila kujua hiyo dawa inakwenda kutibu tatizo gani.

Kwa njia hiyo,utakesha miaka nenda,miaka rudi hauto kaa upone!

Upungufu wa nguvu za kiume lazima utibiwe,kwa kuanzia chanzo cha tatizo;kwa maana ya kwamba mzizi wa tatizo sharti ung'olewe kwanza!

Mathalani, kama tatizo ni la homoni ijulikane kwanza; kama ni tatizo la tezi ijulikane kwanza, kisha matibabu sahihi yaelekezwe katika maeneo hayo.

Hayo ndiyo matibabu, na si vinginevyo.

Upungufu wa nguvu za kiume unaweza kutokana na kisukari kwa mwanume au shinikizo la damu la kupanda (HIGH BLOOD PRESSURE) kwa mwanaume au shida ya tezi dume kwa mwanaume mwingine au shida ya kihomoni (HORMONAL IMBALANCE) kwa wanawake wengine, basi vipi iingie akilini kwamba wote hao watatibiwa na dawa aina moja?

Watu wengi wanaeelewa kimakosa sana,ndiyo maana hata matibabu yamekuwa ni tatizo kubwa sana,kama unahisi una dalili hizo,ni bora uwahi mapema hospital, ukapime kati ya sababu nilizotaja hapo juu kama sio sababu za kuonekana kiurahisi,na ukishabaini chanzo cha tatizo?

Post a Comment

أحدث أقدم
Contact ME
close