Breaking News

 Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kufanya mapenzi kikamilifu au kushindwa kusimamisha vizuri, shughuli ya tendo la ndoa huhusisha akili, homoni, neva, hisia na mirija ya damu, misuli.Tafiti zinaonesha kuwa katika wanaume watano(5) basi mmoja kati yao ana tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Upungufu wa nguvu za kiume huashiria kuto kuwa sawa kiafya hivyo ni tatizo linalo hitaji tiba.

Tatizo hili huwanyima sana watu raha na kupelekea kuwa na mawazo, migogoro katika mahusiano.Watu wenye changamoto hii mara zote wanahitaji dawa zisizo na madhara(virutubisho lishe) vilivyotokana na mimea na matunda na kubadilisha mitindo yao ya kimaisha(Lifestyle changes) ili kuweza kurudisha hali zao na kuondoa tatizo.

Dalili Za Upungufu Wa Nguvu Za Kiume:

Zifuatazo ni baadhi ya dalili za upungufu  wa nguvu za kiume;

1) Kukosa Hamu Ya Kufanya  Tendo La Ndoa.

Tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanaume ni moja wapo ya dalili za upungufu wa nguvu za kiume na linaweza kusababishwa na sababu nyingi sana.Sababu hizo zinaweza kuwa za kimaumbile au kisaikolojia au za mchanganyiko wa sababu za kimaumbile na sababu za kisaikolojia.Baadhi ya sababu za tatizo hili ni pamoja na;

a) Msongo Wa Mawazo (Depression).

Msongo wa mawazo ni ugonjwa wa kisaikolojia unaohusisha hali ya kuwa na mawazo makali kwa muda mrefu yanapolekea kukosa raha kutokana na kujihisi si mtu wa thamani au kukosa starehe katika vitu ulivyozoea kuvifanya na kukufurahisha hapo awali.Mawazo ya namna hii huathiri mwenendo wako wa maisha yako ikiwa ni pamoja na kukosa matamanio ya kimapenzi.

b) Matumizi Ya Madawa Na Pombe.

Matumizi ya baadhi ya madawa na  unywaji wa pombe wa kupindukia vinaweza kupelekea tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.Madawa yanayochangia tatizo hili ni pamoja na;Madawa ya presha ya kupanda(Anti hypertensive drugs), madawa ya kuondoa msongo wa mawazo, madawa yote yanayozuia ufanyaji kazi au uzalishaji wa testosterone, kwa mfano, cimetidine,finasteride na cyproterone n.k

c) Mawazo Mengi Na Uchovu.

Matatizo ya kikazi na hadhi yako kazini vinaweza kuchangia kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.Kama unabezwa sana kazini na kujiona hutimizi kazi yako ipasavyo au kama unachoka sana kazini pia  vinaweza kupelekea kukosa hamu ya kufanya mapenzi pindi urudipo nyumbani kwani mahusiano ya kimapenzi yanahitaji yatengewe muda wa kutosha.

d) Kuwa Na Umri Mkubwa.

Kiwango cha homoni ya testosterone inayohusika na hisia za kimapenzi kwa mwanaume hupungua kwa asilimia 1-2 kila mwaka kadri mwanaume anavyozidi kuwa na umri mkubwa.Kiwango cha testosterone kikishuka katika mwili wa mwanaume humfanya asiwe na nguvu, ashindwe kutuliza mawazo kwenye jambo alifanyalo na apoteze hamu ya kufanya mapenzi.

e) Mahusiano Yaliyopo Baina Ya Mwanaume Na Mwanamke.

Matatizo ya kimahusiano kati ya mwanaume na mwanamke yana mchango mkubwa sana katika kusababisha tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa, mfano uwepo wa migogoro kati ya mume na mke, ukosefu wa amani na furaha katika  mahusiano huchangia sana mwanaume kukosa hamu ya kufanya mapenzi.

Kama mahusiano yako na mpenzi wako yamekuwa ya miaka mingi sana, unaweza kuwa umemzoea mno mkeo kiasi kwamba ukaanza kukosa hamu ya kufanya naye tendo la ndoa.Hili nalo hutokea mara nyingi.

f) Matatizo Ya Kiafya.

Matatizo ya kiafya ya muda mrefu(chronic diseases) husababisha kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa, mfano tatizo la kisukari, tatizo la presha, tatizo la moyo, tatizo la kansa ya muda mrefu, na hali ya kuwa na unene uliozidi kiwango(obesity) n.k

2) Kutokuwa Na Uwezo Wa Kurudia Tendo La Ndoa Zaidi Ya Mara Moja.

Mwanaume mwenye changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume akishakamilisha mshindo mmoja wa tendo la ndoa basi anakua hana uwezo tena wa kurudia mshindo mwingine.Hali hii husababishwa na kutokuwepo na mshukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya uume.

3) Kutokuwa  Na Uwezo Wa Kusimamisha Uume Kabisa.

Kwa kawaida uume wa mwanaume aliyekamilika(rijali) unaposimama, hutakiwa kuwa imara kama msumari, lakini kwa mwanaume mwenye changamoto ya upungufu za nguvu za kiume uume wake hata ukisimama hubakia kuwa lege lege na unaweza kusinyaa wakati wowote.

Tatizo hili ni matokeo ya kulegea kwa mishipa ya uume ambayo ndio huufanya uume usimame barabara.

4) Kuwahi Kufika Kileleni.

Kuwahi kufika kileleni ni hali ambayo inampata mwanaume mwenye changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume ambapo hutoa shahawa kabla ya kuanza tendo la ndoa au muda mfupi tu baada ya kuanza tendo la ndoa, bila yeye mwenyewe kukusudia.Kwa kawaida mtu mwenye tatizo la kuwahi kufika kileleni hutoa mbegu zake za kiume hata baada ya maandalizi kidogo sana.

5) Kuchoka Sana Baada Ya Tendo La Ndoa Na Hata Kukinai Kabisa/Hata Kusikia Kichechefu.

Hii ni moja wapo ya dalili za upungufu wa nguvu za kiume.Hali hii huwapata wanaume wenye changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume ambayo wakati mwingine huambatana na usingizi mzito(Kulala fofofo).

6)  Kuhisi Maumivu Wakati Wa Tendo La Ndoa/Baada Ya Tendo La Ndoa.

Hii pia ni moja wapo ya dalili za upungufu wa nguvu za kiume, hali hii huweza kuchangiwa na kauthirika kwa tishu za uume ambazo hutokana na upigaji wa punyeto kupita kiasi.

7) Kuchelewa  Sana Kufika Kileleni/Kushindwa Kufika Kileleni Kabisa.

Ni ile hali ya mwanaume kuchukua muda mrefu kutoa manii wakati wa kushiriki tendo la ndoa.

Kwa kawaida mwanaume anatakiwa afike kileleni/kutoa manii kwa muda usiozidi dakika 30 wakati wa kushiriki tendo la ndoa.Kwa hiyo mwanaume anaposhiriki tendo la ndoa na kuchukua muda mrefu bila kufika kileleni anahitaji uchunguzi ili kubaini chanzo cha tatizo.

Soma pia hii makala: Fahamu aina 7 za vyakula vinavyo ongeza kiwango cha mbegu za kiume.

Sababu Za Upungufu Wa Nguvu Za Kiume:

Zifuatazo ni baadhi ya sababu za tatizo la upungufu wa nguvu za kiume;

  1. Uzito kupita kiasi na unene uliozidi.
  1. Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi.
  1. Uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe.
  1. Kuwa na mawazo na wasi wasi.
  1. Kuwa na tatizo la kibofu cha mkojo.
  1. Matumizi makubwa ya dawa zenye kemikali za kutibu magonjwa kama kansa, vidonda vya tumbo, kisukari, presha, magonjwa ya moyo nk.
  2. Tabia za kujichua kwa muda mrefu.
  1. Umri hasa wazee.

Njia Za Kuongeza Wingi Wa Mbegu Za Kiume:

Zifuatazo ni baadhi ya njia za kuongeza wingi wa mbegu za kiume;

Upungufu Wa Nguvu Za Kiume

1. Kula Lishe Bora.

Chakula unachokula kina mchango mkubwa katika kutibu tatizo la kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za kiume(Low sperm count).Kama utarekebisha tu aina ya chakula unachokula kunaweza kupelekea kutibu changamoto ya kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za kiume ambapo unashauriwa kupunguza matumizi ya sukari na vyakula vya ngano, badala yake ongeza zaidi matumizi ya matunda, mboga mboga.Hii inaweza kukusaidia kutibu tatizo la kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za kiume kwa haraka sana.

2. Epuka Matumizi Yaliyokithiri Ya Vyakula/Vinywaji Vyenye Kafeini Kwa Wingi.

Kama unasumbuliwa na tatizo la kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za kiume ni  vyema ukaepuka matumizi yaliyokithiri ya  vyakula au vinywaji vyote vyenye kafeini kwa wingi.Mfano wa vyakula/vinywaji vyenye kafeini kwa wingi ni pamoja na chai ya kahawa, soda nyeusi zote, malta, redbull, chokoleti n.k

3.Tumia Kitunguu Swaumu Kwa Wingi. 

Kitunguu swaumu kina ‘Selenium’ na pia kinasaidia kuondoa sumu mwilini, mambo haya mawili muhimu yanasaidia kuongeza spidi ya mbegu za kiume.Pia kitunguu swaumu kina ‘Allicin’ ambayo husaidia kuongeza msukumo wa damu kwenda kwenye uume.Hivyo unashauriwa kuongeza matumizi ya kitunguu swaumu kwenye chakula unachopika.Vile vile unaweza kutafuna punje 2 mpaka 3 za kitunguu swaumu kila unapoenda kulala au unaweza kukatakata(chop)  hizo punje 2 au 3 vipande vidogo vidogo kisha unywe na maji.

kitunguu swaumu

4. Ulaji Wa Ndizi.

Ndizi ni chakula kizuri kwa ajili ya afya ya uume wako.Ndizi zina kimeng’enya kimoja kiitwacho ‘Bromeliad’  ambacho husaidia kuziweka sawa homoni zinazohusiana na tendo la ndoa(testosterone).Pia ndizi zina Magnesium, vitamini B1 na vitamini C, vitu ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya kutengeneza mbegu za kiume.

5. Ulaji Wa Mbegu Za Maboga.

Mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya zinki ambayo ni muhimu katika kutengenezwa kwa mbegu za kiume na homoni ya testosteroni.Pia mbegu za maboga zina vitamini B, C, D, E, na K ambazo zote ni muhimu katika kuongeza idadi ya mbegu za kiume.Vile vile mbegu za maboga  zina madini ya kalsiamu, Potasiamu,Phosphorasi na Niacin.

6. Ulaji Wa Mboga Za Majani Kwa Wingi.

Mboga za majani zinapunguza homoni ya ‘estrogen’ na hivyo kufanya homoni ya ‘testosterone’ ipatikane kwa wingi  na hivyo kupelekea kuongezeka kwa mbegu za kiume.

spinachi

7. Ulaji Wa Vyakula Vyenye Foliki Asidi Kwa Wingi.

Vyakula vyenye  foliki asidi kwa wingi ni pamoja na karoti, Parachichi, Ufuta, maharage, papai, bamia. Hivvyo isipite siku bila kula parachichi walau moja na kutafuna karoti walau moja ikiwa unachangamoto ya kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za kiume.Tafiti zinaonesha kuwa  wanaume walioongeza ulaji wa vyakula vyenye foliki asidi na zinki waliongeza uwingi wa mbegu zao za kiume kwa zaidi ya asilimia 74 kwa muda wa wiki 2 tu.

Matunda mbali mbali yanayo ongeza folic acid

8. Kunywa Maji Mengi Kila Siku.

Hili ni suluhisho rahisi lisilohitaji gharama yoyote  kwa wale wanaosumbuliwa na changamoto ya kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za kiume.Kutokunywa maji ya kutosha kila siku kuna uhusiano wa moja kwa moja na kupungua kwa uwingi wa mbegu za kiume.Hivyo kama utatekeleza njia zote zilizotajwa hapo juu halafu ukasahau kunywa maji hesabu umekosea sana.Kutegemeana na uzito wako unaweza kunywa maji walau lita 2 mpaka lita 3 kwa siku, hii itakusaidia kwani mbegu za kiume zimetengenezwa kwa maji, na pia zipo kwenye hali ya kimiminika.

Maji ya kunywa

9. Parachichi.

Parachichi lina uwezo mkubwa wa kuzalisha vitamin E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni za kiume.Tafiti zinaonesha kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkubwa wa kimapenzi.

parachichi

10. Tikiti Maji.

Matunda haya pia yana uwezo mkubwa wa kuongeza nguvu za kiume.Tikiti lnapaswa kuliwa pamoja na mbegu zake, angalau vipande viwili au vitatu kwa siku.

tikiti maji

11. Komamanga.

Haya ni aina ya matunda ambayo ndani yake yana mbegu nyekundu.Koma manga lina tajwa kuwa na virutubisho muhimu vya kusisimua misuli ya uume na kuamsha hisia za kushiriki tendo la ndoa.

koma manga

12. Pweza Na Chaza.

Aina hizi za  viumbe wa baharini, huwa  na madini ya zinki na chumvi ambayo ambayo yanatajwa kusaidia uzalishaji wa vichocheo vinavyosababisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa.Unashauriwa kujenga utaratibu wa kunywa supu ya pweza mara kwa mara na matokeo yake utayaona.

supu ya pweza

13. Pilipili.

Pilipili zina uwezo mkubwa wa  kumaliza changamoto ya upungufu wa mguvu za kiume.Unaweza kuchangaya pilipili  kwenye chakula au ukala hivyo hivyo kwa kutafuna kiasi kidoogo mara kwa mara.Pilipili zina virutubisho ambavyo husaidia kuongeza msukumo wa damu kwenye mishipa ya uume na kuamsha hisia za mapenzi.

14. Kunazi(Blueberries).

Haya ni matunda madogo madogo jamii ya zabibu ambayo huliwa na binadamu.Matunda haya yameelezwa kuwa na nguvu kama ilivyo dawa ya Viagra.Tafiti za kitaalamu zinaonesha kuwa matunda haya yana vichocheo ambavyo hulainisha mishipa ya damu na kufanya damu isambae kwa kasi kuelekea kwenye viungo vya kiume.

15. Ufanyaji Wa Mazoezi Mara Kwa Mara.

Mazoezi ya nusu saa mara tatu kwa wiki kwa wanaume yana uwezo wa kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mbegu za kiume kwa mujibu wa wanasayansi ambapo wanaume ambao wameendelea na zoezi la kukimbia kila wakati, mbegu zao za kiume huwa na afya njema kulinganan na watafiti wa jarida la maswala ya uzazi.Watafiti wanasema ni muhimu kufanya mazoezi hayo kwa kiwango cha wastani, kwa sababu mazoezi ya kupita kiasi hudhuru kiwabgo cha uzalishaji wa mbegu hizo za kiume.

Mazoezi ya kukimbia

HITIMISHO:

Ikiwa unasumbuliwa na changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume unashauriwa kufanya mazoezi angalau dakika 30 kwa siku, Kula vyakula asilia na usipendelee kula vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi, Tibu magonjwa yanayokuweka hatarini kama kisukari, magoonjwa ya moyo, punguza unene uliozidi, lala vizuri kwa muda mzuri masaa 7 hadi 9, Epuka uvutaji wa sigara na matumizi ya pombe yaliyothiri, kunywa maji ya kutosha n.k

Post a Comment

أحدث أقدم
Contact ME
close