Breaking News

Hivi ni kweli wanaume wanachepuka kwakua Mwanamke kazaa, ana mabadiliko katika mwili wake, kazeeka au hajui kufanya mapenzi kama vibiti vidogo? 

Je kuna vitu ambavyo mwanamke anaweza kuvifanya ili mwanaume ambaye anachepuka asichepuke tena? 

Kama kuna kuzeeka na wanaume wanachepuka kwakua wanawake wamezeeka je kuna ndoa iko salama? 

Vipi mwanamke afanye nini ili mume wake asichepuke?

Najua hili ni swali ambalo wanawake wengi hujiuliza sana, mwanaume anapoanza kuchepuka basi mwanamke huanza kujiangalia maumbikle yake, kuona kama kazeeka, kuona kama kabadilika na vitu kama hivyo. Wanawake wengi huchanganyikiwa, wanakua hawajiamini na kujikuta kila siku wakijilaumu wao, lakini je ni kweli kuna ukweli hapo, kuna baadhi kuna ukweli na kwa kiasi kiukubwa hakuna ukweli, hembu tuendelee kidogo.

(1) Tamaa; Hii ni sababu kubwa ya wanaume wengi kuchepuka, yaani anachepuka kwakua kaona mdada ana tako kubwa tu, kaona mdada anajichekesha chekesha tu, mdada kajileta mwenyewe, anatamani anachepuka na wala hata hana sababu ya maana. Mwingine unakuta kaoa binti mzuri mkali anaenda kuchepuka na mwanamke ambaye hata hafikii nusu yake kisa tu katamani nywele zake, katamani namna anavyoongea, anavyojiamini au kuma mshikaji kamsifia tu kuwa yaliyomo yamo!

(2) Mwanamke kuwa na Kisirani; Hii kitu inachepusha wanaume wengi tena ni mbaya zaidi kwakua mwanaume anayechepuka kwakua ana tamaa basi hurudi ila anayechepuka kukwepa kisirani basi huyu analowea kabisa mpaka unahisi kalishwa limbwata. Mwanaume anaweza kuwa anampenda mke wake, hana hata tamaa, kashamaliza kufanya mambo yake lakini akirudi nyumbani simu inakaguliwa mpaka utumbo, mtu kanuna tu kwakua kuna mtu kalike picha yake, umetoka kazini umechoka mtu anakukumbushia minuno ya wiki iliyopita, hapa ni ngumu mwanaume kugeuka nyumba yaani analazimika tu kukaa nnje ili achelewe kurudi na akikutana na mtu ambaye anajua kucheka basi wanacheka wote.

(3) Mwanamke Kutokujiamini; Hapo tunakuja kwenye suala la umri, sura na vitu kama hivyo, mwanamke unapokua hujiamini unaboa kila saa kujilinganisha, mara nimezeeka, mara sina tako, sina hiki, sina kile. Umekaa na mwanamke, wakati unamkuta hukumkuta na tako lakini kila akipita mwanamke na tako lake basi kanuna, hasira akikuona na mwanamke ambaye anahisi kamzidi kitu basi ananuna na kuhisi kadharauliwa. Una watoto wa nne una wasiwasi kuwa umeharibika, kwani ulitegemea nini, uwe na watoto halafu uwe vilevile, jiamini.

(4) Mwanaume Kutokujiamini; Kuna wanaume wengi wanachepuka ili tu kuwachoma roho wake zao. Hawafurahii kuchepuka, hakuna cha maana wanachotata huko, lakini labda kwakua kaoa mwanamke mzuri, kaoa mwanamke ana pesa kuliko yeye, kaoa mwanamke ana elimu kuliko yeye au mwanaume kitandani hayuko vizuri, iwe ni maumbile au hapigi mecho muda mrefu. Basi anahisi mke wake anachepuka au anamdharau hivyo ili kumuonyesha kuwa hata kama hunipendi kuna ambao wananipenda.

Basi unakuta anachepuka, chepuka ya huyu ni ya dharau, mwanaume ambaye hajiamini akichepuka atataka mke wake ajue, atamuonyesha, ataacha meseji za wanawake wengine, mapicha, akifumaniwa hata haombi msamaha, kibaya zaidi anatukana na kudhalilisha, na mwanamke akitaka kumuacha hataki, atang’ang’ania watoto au kuomba msamaha ila habadiliki, huyu ni kujiamini hajiamini wala sio umalaya! Anataka tu kumuonyesha mwanamke kuwa hata ukiniacha kuna wengine ili tu mwanamke asijiamini awe mtumwa wake.

(5) Mwanamke kutokuheshimu Tendo la ndoa; Sababu kubwa ya ndoa ni tendo la ndoa, wanawake wengi wakishazaa au wakifikia umri flani unakuta wanakinahi tendo la ndoa, sasa anafanya tu kama vile ni wajibu na haliheshimu kujua kuwa yanahitajika madoido na manjonjo mengi ili kufanikisha hili tendo. Hakuna ubunifu mwanaume anakugusa ni kama unasema fanya ukimaliza niambie.

Wengine unakuta hata kutaka kufanya mapenzi hawataki, mwanaume yuko vizuri ila kila siku umechoka. Aisee hapa mwanaume atachepuka tu, atajaribu kukuelewesha siku ya kwanza, yapili ila ya tatu atatafuta mwingine. Ndiyo maana nakuambia, kama kazi zinakuosha tafuta binti wa kazi kukusaidia kazi za nyumbani ili kazi za chumbani zisikuchoshe kwakua mwanaume akioa hataki kubembelezea penzi kama anatongoza upya!

(6) Kumchunguza chunguza Mwanaume; Najua unaweza kushangaa lakini kuna wanawake wengi wanaishi kwenye ndoa za mateso wakidhani waume zao ni malaya kumbe wala hawachepuki. Kila dakika umeshika simu ya mume wako, ukiona namba ya mwanamke unapiga mara achana na mume wangu, hutaki awe na marafiki wakike. Mmetoka out akikumbatiana na mdada wa ofisini ushanuna na kumchepusha.

Ukiona meseji nimekumiss basi ushachanganyikiwa unapiga na simu. Akitoka out na mwanamke ushanuna, basi hii hata kama mwanaume hachepuki utaishia kuumia tu. Ukimfuata fuata mwanaume namna hii atafikiri unataka kumkalia kichwani, unamuona mjinga na mbaya zaidi wanaume hatupendi kukaliwa kichwani wlaa kupangiwa maisha. Anaweza asichepuke lakini akaamua kukuumiza tu kuwa kile unachomkataza kila siku basi akawa anakifanya ili tu kukuumiza na kukuonyesha kuwa yeye ndiyo mwanaume.

(7) Kila mwanaume ukimchunguza sana anchepuka; Nimalizie kwa kusema Dada zangu huwezi kumdhibiti mwanaume na kama ukimchunguza sana basi utaamini anachepuka hata kama hachepuki. Kuna mwanamke kazoeana naye tu lakini si mpenzi wake, kuna mfanyakazi wanataniana taniana ila si mpenzi wake, kuna X wake alishamuacha ila X hakubali anakurusha roho kwakua umeolewa wewe na vingine vingi hivyo kama huna uwezo wa kumuacha mwanaume wako, kaa kwa kutulia acha kumfuatilia.


Post a Comment

أحدث أقدم
Contact ME
close