Breaking News

 




Mambo 10 usiyoyajua kuhusu watoto wachanga.

Makala haya yameandaliwa kutokana na mahojiano yaliyofanyika kati ya mtaalam wa afya ya watoto kutoka katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Malawi – Blantyre (Malawi University College of Medicine).

1. Choo chao cha kwanza huwa hakinuki.

Choo chao cha kwanza chenye muonekano wa kama lami, kina ute na majimai kutoka tumboni pamoja na chochote kile wanachokuwa wamekula wawapo tumboni mwa mama zao na mara nyingi choo hiki huwa hakinuki. Huwa bado hakijapata bakteria wa tumboni ambao hufanya choo kinuke. Lakini kitaanza kunuka punde baada ya bakeria kuenea tumboni. Baada ya siku moja au mbili choo chake kinakuwa cha kijani kisha cha njano na baadae rangi ya hudhurungi ambayo ni rangi yake asili.

2. Huwa wanalia bila machozi, kwa mara ya kwanza.

Watoto wachanga wana anza kulia kuanzia wiki ya 2-3 lakini machozi yana anza kutoka baada ya kuwa wamefikisha mwezi mmoja. Wakati wa alasiri na jioni ndio wakati wanaopenda kuwa wasumbufu, bila sababu ya msingi na hakuna utakachoweza kufanya kuwatuliza.

"Kipindi cha watoto kulialia zaidi" ni katika wiki ya 46 hivi baada ya kujifungua au mtoto akiwa na wiki 6 mpaka 8 kwa watoto waliozaliwa wakiwa wametimiza umri wa kuzaliwa. Baada ya miezi 3, tufani huwa imepita.

3. Wakati mwingine watoto wachanga wanaweza kuacha kupumua kwa muda.

Watoto wachanga wanaweza kuacha au kukoma kupumua kwa sekunde 5 mpaka 10 hususani wanapokuwa wamelala kitendo ambacho hutosha kumfanya mzazi yeyote yule kuchanganyikwa. Ila huna sababu ya kutahayari, lakini kama mwanao atakoma kwa muda mrefu zaidi au kama atabadilika na kuwa wa bluu. Hiyo ni dalili ya hatari, tafuta msaada wa kitabibu haraka iwezekanavyo.

Lakini kama hali hii pia inaweza kujitokeza baada ya motto kushtushwa au baada ya kulia.

4. Watoto wa kiume huwa wanasimamisha uume wao.

Kitendo ambacho mara nyingi huwa kinatokea  pale anapokuwa anataka kukojoa. (Hii inaweza kuwa ni dalili nzuri ya kuangalia kama mtoto ni mzima).

Unaweza kuona wakati unapokuwa ukimbadilisha mwanao daipa, nepi ama kumpeleka kujisaidia. Sababu hasa ya kusimamisha uume wakati wa kukojoa haijulikani, hata hivyo siyo jambo la kutahayari au kuonea haya. Unaweza kuona hili kupitia kipimo cha ultrasound kabla mwanao hajazaliwa.

Uume wake unaweza kuonekana mkubwa wakati wa kuzaliwa, hata hiyo pia ni jambo la kawaida.

5. Watoto wachanga huwa matiti makubwa.

Wanapozaliwa kwa mara ya kwanza wote watoto wa kiume na kike huwa wanaonekana kama wana matiti makubwa kuliko inavyotarajiwa.

Na wakati mwingine matiti haya huwa yanatoa maziwa.

Kwenye chuchu zao kumefanyika vibonge, kwa sababu ni vichocheo vya estrogeni kutoka kwa mama na vitapotea vyenyewe baada ya wiki chache.

Pia kwa  Watoto wa kike wanaweza kuwa wanatokwa na hedhi ndogo au maji maji kutoka ukeni nayo hayo yatapotea baada ya siku chache.

6. Mafindofindo (tonsils) yao yanakuwa yana tezi kwa ajili ya kutambua ladha ya chakula.

Mtoto mchanga anakuwa na tezi za kutambua ladha ya chakula, ambazo huwa na ukubwa sawa na zile walizonazo vijana wadogo.

Tofauti kubwa ni kuwa tezi za vichanga zimechukua eneo kuwa zaidi hadi kufika kwenye mafindofindo hadi nyuma ya koo. Mtoto mchanga anaweza kuonja vitu vitamu, vichungu, vichachu ila bado hawezi kuitambua ladha ya chumvi kwani ladha hii ni mpaka miezi mitano.

7. Hupenda kulala kuelekea upande wa kulia.

Ni asilimia 15 ya watoto wachanga wanaopenda kuelekeza uso wao upande wa kushoto wanapaolalia mgongo. Inaoenekana ina uhusiano na jeni (gene) kama ilivyo kwa kitobwe(dimples). Tabia hii ya kupenda kulala kuelekea upande wa kulia inachukua miezi kadhaa kabla ya kupotea, na hata hivyo inaweza pia kusaidia kuelezea kwa nini watu wengine ni mashoto au wengine hutumia mkono wa kulia.

8. Wana kiwango kikubwa cha baadhi ya seli za ubongo.

Ubongo wa mtoto mchanga utakuwa mara mbili zaidi katika mwaka wa kwanza. Ubongo huu unakuwa tayari una seli za neva nyingi zaidi ya zile za mtu mzima ambazo zina uwezo wa kubeba taarifa za fahamu. Seli nyingi huwa zinakufa na seli chache zinazalishwa.Na baada ya kuwa mtu mzima unajikuta una seli chache za neva kuliko ulivyokuwa mtoto. Na muunganiko kati ya seli moja na nyingine huwa unapunguzwa kitu ambacho husaidia kuongeza umakini lakini hunapunguza ubunifu.

Watoto ni wabunifu kuliko watu wazima.

Hili   Halipingiki.

9. Wanaweza kujishitua wenyewe.

Siyo jambo gumu kushituka kwa mtoto mchanga: - sauti kubwa, harufu kali, mwanga mkali, mtikisiko wa ghafla na hata kulia kwao wenyewe kunaweza kuwashitua. Utajua hivyo vyote pale atakapokuwa akitupa mikono yake pembeni huku akiwa amekunjua viganja vyake kisha kwa haraka akikunja vinganja vyake na kuipeleka nyuma ya mwili wake.

10.                  Baadhi ya alama za kuzaliwa zitapotea.

Alama ya kung'atwa na korongo (Stork bites) au "busu la malaika" la rangi nyekundu au pinki mara nyingi kwenye paji la uso, kwenye kope za macho au kwenye sehemu ya nyuma ya shingo ikiwa ni pamoja na doa la kimongolia - doa la bluu ambalo huonekana kama wino uliovia mgongoni au kwenye matako. Hili hupotea ndani ya miaka michache. Chanzo chake hakijulikani.

Alama ya rangi nyekundu iliyokolea kama ya stroberi hutokana na mishipa ya damu inayokua kwa kasi. Hizi alama hutokea baada ya wiki nyingi na huchukua miaka kadhaa kupotea.

Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116 ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa 

 

 

Post a Comment

Previous Post Next Post
Contact ME
close