Breaking News

 Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu Afunguka Utata wa Wakurugenzi Wawili Katika Uteuzi, 54 Watumbuliwa

Udaku SpecialAug 3, 2021


Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu amewataka Wakurugenzi wote wateule wakaripoti kwenye vituo vyao vya kazi kupitia kwa Makatibu Tawala wa Mikoa ndani ya siku tano kuanzia kesho na makabidhiano ya Ofisi yafanyike mara moja.


“Wakurugenzi wawili ambao majina yao yameonekana kutokea kwenye maeneo zaidi ya moja wataripoti kwenye kituo ambacho jina limeonekana kwa mara ya kwanza kwenye orodha ya uteuzi, aidha pale palipojirudia jina patatambulika Kama nafasi wazi na itajazwa hapo baadaye”——— Ummy Mwalimu


Samia Atumbua Wakurugenzi 54



Samia atumbua wakurugenzi 54


WIZARA ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetoa siku tano kuanzia leo kwa wakurugenzi wapya wa majiji, manispaa, miji na halmashauri za wilaya wafi ke kwenye vituo vya kazi kuanza kutekeleza majukumu yao.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Ummy Mwalimu amewataka wakurugenzi hao waende kuripoti kwa makatibu tawala wa mikoa kwenye mikoa husika.


Rais Samia Suluhu Hassan juzi ameteua jumla ya wakurugenzi 184, na kwa mujibu wa Ummy, 70 kati ya hao wamehamishwa kutoka vituo vyao vya kazi na 45 wamebaki walipokuwa.


“Aidha, katika idadi hiyo wakurugenzi 69 ni wapya wakiwemo 15 walioteuliwa kujaza nafasi 54 zilizoachwa wazi baada ya waliokuwa wakurugenzi katika nafasi hizo kutenguliwa,” alisema Ummy alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. Ummy alisema miongoni mwa wakurugenzi wapya, 33 sawa na asilimia 48 ni wanawake na hivyo kufanya idadi ya jumla ya wanawake wakurugenzi kufikia 55 sawa na asilimia 29 ya wakurugenzi wote nchini.


Alisema wakurugenzi wawili ambao majina yameonekana kutokea kwenye maeneo zaidi ya moja wanapaswa kwenda kuripoti kwenye kituo ambacho jina limeonekana kwa mara ya kwanza kwenye orodha ya uteuzi.


Alisema pale ambapo jina limejirudia patatambulika kama nafasi wazi na itajazwa baadaye na akazitaja nafasi hizo ni Halmashauri ya Mji wa Misungwi na Njombe.


Ummy aliwataka wakurugenzi ambao uteuzi wao umetenguliwa waende kuripoti kwa makatibu tawala wa mikoa waliyokuwa wakivifanyia kazi ili wapangiwe majukumu mengine kwa kuwa bado ni watumishi wa umma

Post a Comment

أحدث أقدم
Contact ME
close