Kila mwanamke huwa kuna kipindi flani katika mzunguko wa mwezi hupitia katika hali ambayo wanakuwa katika hedhi. Jambo hili kwa kawaidi huchukua kipindi cha kati ya siku 3 hadi 7 kulingana na maumbile. Pia kila mwanamke hupitia wakati huu kwa kuwa na hali tofauti na mwingine hivyo hedhi za mwanamke mmoja huwa tofauti na za mwanamke mwingine.
Hoja ya leo tumekuja na mambo ambayo hupaswi kumwambia mwanamke ambaye yuko katika hedhi. Mwanaume kwa kawaidha hedhi huonekana ni jambo la kawaida tu lakini kwa mwanamke huwa na uzito mkubwa hivyo kama mwanaume, ukiingia kwa mahusiano na mwanamke lazima uwe na umakini mkubwa haswa wakati mpenzi wako anakuwa katika siku zake.
Tumekusanya maoni ambayo yanajumlisha mambo ambayo hupaswi kumwambia mwanamke anapokuwa katika siku zake.
Zama nasi…
Mambo hupaswi kumwambia mwanamke akiwa katika hedhi
#1 Umeingia kwa siku zako ama ni nini?
Wanawake hujulikana kuwa wanapoingia katika siku zao mara nyingi wanakuwa na hisia za ukali. Hivyo hupaswi kuchukua hatua ya kumuuliza swali hili kwa kuwa unamwona amekuwa tofauti kihisia. Wanawake hawapendi hili jambo. [Soma: Maswali mazuri ya kumuuliza mwanamke]
#2 Nenda ukameze dawa ya maumivu.
Dawa ya maumivu si suluhu ya maumivu ambayo wanapitia wakiwa katika hedhi. Hivyo hata akiamua kumeza hio dawa ya maumivu wakati huo haitamaliza uchungu wake na dakika moja.
#3 Unataka kisodo ama kitu gani?
Swali hili kwako unaweza kuliona rahisi lakini kwa mwanamke huchukulia kwa uzito flani. Kwake ataona kwamba unamfanya dhaifu kwa kutumia kisodo.
#4 Maumivu ya hedhi hayaumizi sana
Maoni yako hapa hayahitajiki maana hujui hali halisi ambayo anapitia wakati ameingia kwa siku zake.
#5 Ongea na mimi baada ya hedhi zako kuisha
Well, fikra za kukwambia usiongee na yeye tena zitakuwa zinamzunguka kichwani lakini hana la kukuambia. [Soma: Hatua za kuchukua kumshawishi mwanamke mfanye mapenzi]
#6 Acha kulalamika.
Pia hapa mwanamke hapendi kuambiwa hivi maana hedhi kwake ni jmbo ambalo amekuwa akilipitia kwa miezi mingi sana.
#7 Nikikununulia chocolate itakusaidia?
Badala ya kumwambia mambo kama haya ni bora utafute kitu ambacho kitakuwa na manufaa ya kudumu kwake.
#8 Si ubadilishe hio nguo umevaa.
Hapa yuko katika nyakati za maumivu hivyo mwache ajiskie huru na kile ambacho anajiskia nacho.
#9 Sasa nimejua kwa nini wakati ule wote ulikuwa umebadilika.
Wanawake wote wakiwa katika hedhi huwa wanabadilika so si ishu kubwa ya kuongea.
#10 Uchafu
Ukiwambia hivi mpenzi wako basi inamaanisha haujakomaa kuingia katika mahusiano.
#11 Mbona unalia?
Ukimuuliza swali hili tarajia jibu la ‘sijui nalia kwa nini’ [Soma: Hatua za kutambua kama mwanamke ana boyfriend]
#12 Afadhali haukupata uja uzito
Swala kama hili linawakera wanawake wakiwa katika siku zao.
#13 Unatumia vibaya hii fursa kuwa na hasira zisizokuwa na msingi.
Mwanamke akiwa katika hedhi kawaida huwa hayuko katika hali yake ya kawaida hivyo hawezi kuwa anajifanya.
#14 Ujue na mpema sikununulii kisodo/pedi
Hapa kama hutaweza kumnunulia mpenzi wako kisodo basi ina maana haujakomaa, bado wewe unafikra za kitoto.
#15 Ni siku kidogo tu itaisha, si vibaya.
Usijaribu kuleta hoja kama hii kwa kuwa si vizuri. Wanawake hupitia changamoto nyingi kuanzia haswa ikija katika maswala ya uzazi so haina haja kuongea mambo ambayo huyawezi kuyahimili.
Ok. Haya ni baadhi ya mambo ambayo umeweza kuyakusanya na ambayo hupaswi kumwambia mwanamke yeyote. Kama unaweza kuongeza mengine ingia kwa comment section uyaeleze.