Breaking News

  Ushawahi kujiuliza ni kwa nini mwanamke anakuwa na mood tofauti tofauti katika maisha yake? Leo unaweza kumpata ana furaha, kesho huzuni ama kesho kutwa akikuchukia. Well, haya yote huletwa na mzunguko wa hedhi yake. Wanawake wanakuwa na mduara wa kila mwezi ambao huwabadilisha badilisha kitabia kulingana na homoni zao mwilini.


Lakini mada hio tutaizungumza wakati mwingine. Leo tunataka kujua zile siku ambazo mwanamke huwa na uchu mwingi zaidi kuliko zile siku nyingine.


Je, unataka kujua zile siku ambazo kuna uwezekano mkubwa kwa mwanamke kufanya mapenzi na wewe zaidi kuliko siku zake nyingine


Zama nasi, hapa Nesi Mapenzi tutakueleza kwa kina.


Ni siku gani ambazo mwanamke anakuwa na uchu mwingi?


1. Wakati ambapo anaachilia mayai yake (ovulation)

Mwanamke huwa na uchu mwingi wakati wake wa ovulation kwa sababu huu ndio wakati mwafaka wake wa kushika uja uzito. Wakati huu homoni zake huwa juu zaidi ya siku nyingine yeyote ile hivyo yuko tayari kujamiiana.

Lakini fahamu ya kuwa haimaanishi mwanamke atakubali kujamiiana na mtu yeyote kwa sababu homoni zake ziko juu, la. Mwanamke akiwa katika siku zake wakati huu anaweza kuwa huru kujamiiana na mpenzi wake zaidi. [Soma: Mbinu za kutambua kama ana uume mkubwa]


2.  Mwezi wa nne baada ya kupata uja uzito.

Wakati mwanamke amepata uja uzito, huwa kuna uongezeko mkubwa wa homoni ya estrogen na progesterone. Homoni hizi huchangia pakubwa kwa mwanamke kuongezeka kwa hamu ya kujamiiana. Lakini kwa kuwa wakati huu mwanamke hupitia changamoto nyingi za uja uzito kama vile kutapika, kisunzi na hali nyingine nyingi ambazo hajazizoea (morning sickness), kawaida hamu ya tendo la ndoa hufichika.

Lakini akishazoea hali hii (hutokea baada ya miezi mitatu hadi minne), hamu ya kujamiiana huongezeka mara dufu.


3. Wakati anapopata hedhi.

Wakati huu pia mwanamke huwa na hamu ya tendo la ndoa. Hii haitaonekana kawaida kwa sababu huu ndio wakati wa chini kabisa ambapo mwanamke hawezi kupata uja uzito. Ukweli ni kuwa hamu ya kufanya tendo la ndoa huongezeka kwa sababu mwili wa mwanamke wakati huu unajisafisha kwa kuondoa mayai ambayo hayakuweza kupewa virutubishi kutoka kwa manii ya mwanaume. [Soma: Mambo ambayo mwanamke hataki kuambiwa akiwa katika siku zake]


4. Anapoanza menopause.

Menopause ni wakati ambao mwanamke anapoteza uwezo wake wa kupokea hedhi za kila mwezi. Wakati huu mwili wa mwanamke huanza kuchakatua homoni zote ambazo zilikuwa zimehifadhiwa kabla kusitisha kufanya kazi na kuingia katika hatua nyingine ya menopause.

Wakati huu mwanamke hupatwa na msisimko wa kujamiiana ambao huchukua muda wa siku hadi miezi kadhaa. [Soma: Sababu zinazowafanya wanawake kuchepuka]

Post a Comment

Previous Post Next Post
Contact ME
close